 |
P-FUNK MAJANI |
KUTOKANA na kuwa na upungufu wa maprodyuza kwa miaka ya 1990 hali
ilisababisha kunishawishi kuwa prodyuza ili kuutambulisha muziki wa
Tanzania katika mataifa mbalimbali nje ya fani ya kutengeneza muziki, ni
muimbaji mzuri hususani wa Hip Hop hayo ni maneno yaliyokuwa
yanazungumzwa na prodyuza Paul Matthysse anayejulikana kwa jina la P
Funk Majani alipokutana na ISMAIL NIYONKURU wikii hii
Alianza kupenda kufanya muziki mwaka 1992 huku akiwa ameunda kikundi cha
muziki kilichokuwa kinajulikana kwa jina la 'Street Wisdom' kwa kipindi
hicho alitumia muda wake mwingi kufanya muziki kwani ndio kitu
alichokuwa akikipenda
Alikuwa anapenda kuimba muziki wa Hip Hop kwa kipindi hicho cha miaka ya
90, ingawa kwa sasa ni produza anamiliki studio ya Bongo Records, huku
akibainisha kuwa studio hiyo imewatoa mastaa wengi akiwemo msanii Juma
Nature na wengine wengi
 |
P-FUNK |
Kutokana na hali ya kupenda kufanya Hip Hop alijikuta analazimika
kubadili fani na kuingia katika prodyuza huku akiwa na ndoto lukuki za
kutengeneza muziki wenye ubora wa kimataifa na kuutangaza muziki kwenye
ngazi ya kimataifa
Kwa kipindi chote hicho aliweza kufanikiwa kwa asilimia kubwa
kuutambulisha muziki hapa nyumbani na kuleta changamoto tofauti hali
iliyosababisha mapokeo ya muziki huo kuwa mazuri na mashabiki kuukubali
muziki wa bongo fleva
Alianza safari ya kuwa produza mwaka 1997 wakati ambao watu wengi
hawaelewi muziki na kulikuwa na dhana tofauti tofauti huku baadhi ya
watu wakidai anayefanya muziki ni muhuni wengine wakidai muziki ni wa
watu furani kwenye jamii
Aliweza kung'araa zaidi alipokuwa Produza kwa kukuza vipaji vya wasanii
wengi na kuufanya muziki wa Tanzania uweze kujulikana ndani na nje ya
nchi huku akibainisha kwamba albamu ya Feruz Mrisho iliyobeba jina la
Starehe ndiyo iliyoongoza kwa mauzo kwa kufikia nakala 500,000 katika
wasanii wote waliokuwa kwenye lebo yake
Hakuwa nyuma kwa kuwa na mikakati ya kuufanya muziki utambulike kwani
alikuwa ni mtu ambaye anaweza kuandaa 'concert' za uzinduzi wa albamu
mbalimbali za wasanii waliokuwa chini ya lebo yake na aliweza kufanikiwa
kwa kiasi kikubwa kwani mpaka sasa hakuna msanii aliyeweza kuipita
rekodi ya Juma Nature wakati wa uzinduzi wa albamu yake ya Ugali
alipoweza kujaza mashabiki katika ukumbi wa Diamond
 |
P-FUNK NA TUZO YA KILI MUSIC |
Mikakati hiyo bado anaendelea nayo kwa kuwaomba wadau wa muziki
wajitokeze kudhamini shoo hizo kwani wananchi na mashabiki bado
wanahitaji kuona wasanii wao wanafanya uzinduzi wa aina hiyo, hali hiyo
itasababisha kuepusha wasanii kufanya uzinduzi wa single zao katika
club huku idadi ya mashabiki wakizidi kupungua siku hadi siku
Kwa sababu ya kupenda kuimba muziki wa Hip Hop mwaka jana prodyuza Pfunk
aliamua kufufua kundi la muziki linaloundwa na watayarishaji wakali wa
muziki wa bongo fleva akiwemo John Mahundi, Lamar huku wakiwa wameachia
single yao inayojulikana kwa jina la 'No Name'
Siku za mapumziko anapenda kwenda ufukweni kupunga upepo huku akiamini
kuwa mawazo mapya na ubunifu mwingine anaupata akiwa katika maeneo hayo
ya ufukwe
Anapenda sana rangi nyekundu na huchagua rangi nyekundu kwenye mavazi
yake huku akiamini kuwa rangi hiyo humaanisha hatari ingawa si hatari
kwenye maisha yeake